Nembo ya AFYA KWANZA Hospital

AFYA KWANZA HEALTH FACILITY

“Afya Yako Ndiyo Furaha Yetu”

Taarifa kwa Wagonjwa

Karibu AFYA KWANZA Hospital. Tunawahudumia wagonjwa wetu kwa upendo, heshima na weledi wa hali ya juu. Lengo letu ni kuhakikisha kila mgonjwa anapata huduma sahihi kwa wakati na katika mazingira salama.

Jinsi ya Kupata huduma

Utaratibu wa mapokezi na huduma zinavyo tolewa AFYA KWANZA Hospital, mgonjwa au ndugu yake anatakiwa kufuata hatua zifuatazo:

  1. Kufika katika idara ya mapokezi (Reception/OPD) kwa kisikilizwa maelezo yake.
  2. Kupimwa na daktari ili kujua chanzo cha tatizo la mgonjwa na kiwango cha kuathirika kwake na kutoa mwongozo wa kulazwa endapo itahitajika au kuruhusiwa.
  3. Kukamilisha usajili wa mgonjwa katika kitengo cha kulazwa.
Kumbuka: Wagonjwa wa dharura hupokelewa moja kwa moja bila kuchelewa kwa ajili ya huduma ya haraka ya kuokoa maisha.

Ujumbe kwa Wagonjwa Wetu

Tunafurahia mwanzo wa matibabu ya mteja wetu uwe katika usimamizi wetu wenyewe kwa umakini na weredi ili kuto kukosea.
Tunawashukuru kwa kuchagua AFYA KWANZA Hospital. Afya yako ni kipaumbele chetu cha kwanza. Tumejizatiti kuhakikisha kila mgonjwa anapata huduma bora, salama na yenye heshima.